KILI STARS YAZIDI KUFANYA VIBAYA YAPIGWA 2-1 NA RWANDA.
- Rehema Lucas
- Dec 9, 2017
- 1 min read

Timu ya Tanzania bara Kilimanjaro Stars imepoteza imani ya kwenda nusu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge baada ya kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Rwanda mchezo uliochezwa leo kwenye uwanja wa Jomo Kenyatta mjini Machakos, Kenya.
Kipigo hicho kinamaanisha Kilimanjaro Stars imekwishatolewa na sasa itaingia kwenye mchezo wa mwisho dhidi ya wenyeji, Kenya Desemba 11 kukamilisha ratiba .
Kili Stars ilianza michuano kwa sare ya 0-0 na Libya kabla ya kufungwa 2-1 na Zanzibar na leo pia wamefungwa 2-1 na Rwanda.
Hadi mapumziko, timu hizo zilikuwa zimekwishafungana bao 1-1, Kipindi cha pili, Rwanda walirudi na mbinu mapya na nguvu zaidi hadi kufanikiwa kupata bao la ushindi lililofungwa na Abeid Biramahire dakika ya 65 akimalizia krosi ya Omborenga Fitina.
Kilimanjaro Stars inayofundishwa na Ammy Ninje ilipambana mno kusaka bao la kusawazisha, lakini waliishia kupoteza nafasi chache walizotengenza.
Comments