top of page

WANAFUNZI 650,000 WAJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA

  • Khalidi
  • Dec 8, 2017
  • 2 min read

Wanafunzi 650,852 sawa na asilimia 98.31 ya waliofaulu mtihani wa darasa la saba wamechaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza katika awamu ya kwanza ya mwaka 2018

Wakati hao wakipata nafasi wengine 11,173 sawa na asilimia 1.69 ya walioaulu wamekosa nafasi ya kujiunga na kidato cha kwanza katika awamu hiyo kwenye shule za Serikali kutokana na uhaba wa miundombinu

Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na serikali za mitaa, Selemani Jafo, aliwaambia waandishi wa habari kuwa wanafunzi waliofaulu mtihani wa darasa la saba mwaka huu ni 662,035 sawa na asilima 72.75 ya waliofanya mtihani

Alisema wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu imeongezeka kwa wanafunzi 124,209 sawa na asailimia 223.58 ikilinganishwa na wanafunzi 526,653 waliochaguliwa awamu ya kwanza kujiunga na kidato cha kwanza mwaka jana

Aidha alisema kwa mwaka huu wanafunzi wote 1,912 wenye mahitaji maalum waliofaulu mtihani wa darasa la saba wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka 2018 kwenye shule za sekondari za serikali

Kuhusu waliokosa nafasi, Jafo alisema wanafunzi hao hawajapata nafasi kutokana na uhaba wa miundombinu ya elimu hususani vyumba vya madarasa kwenye baadhi ya mikoa

Alitaja mikoa hiyo na idadi ya wanafunzi waliokosa kuwa ni Lindi (170), Mbeya (3,092), Rukwa (4,091) Manyara (1,268), Katavi (976) na Simiyu (1,576)

“Halmashauri ambazo zimeshindwa kuwapangia wanafunzi wote waliofaulu nafasi ya kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2018 katika awamu ya kwaza ni Lindi (170), Chunya (80) Mbaeya (207), Jiji la Mbeya (1,227) Mbarali (1,578), kalmbo (166), Nkasa (1,318), Sumbawanga (1,553), na Babati (581)” alisema Jafo

Jafo alizitaja Halmashauri zingine kuwa ni Hanang (687) Mpanda (262), Nsimbo (714), Mji Baridi (369) na Busega (1,207)

Jafo alisema katika kuhakikisha wanafunzi hao wanapata nafasi, amewaagiza wakuuu wa mikoa husika kuhakikisha wanafunzi wote wanapata nafasi ya kujiunga na kidato cha kwanza.

Comments


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page