top of page

WAATHIRIKA BOMOABOMOA WAPATA OFA YA KRISMASI.

  • Khalidi
  • Dec 7, 2017
  • 1 min read

Ofisi ya mkoa ya wakala wa barabara (Tanroads) imeamua kusimamisha ubomoaji wa nyumba 1200 zilizopo eneo la kati ya ubungo na kimara kwa kipindi cha kuelekea sikukuu za krismasi na mwaka mpya.

Nyumba ni zile ambazo zimejengwa mita 91 kutoka barabara ya morogoro ikiwa ni mwendelezo wa awamu ya pili ya ubomoaji wa ziaidi ya nyumba 1000 zilizokuwa ndani ya hifadhi hiyo ya Barbara hiyo . tayari nyumba zilizokuwa ndani ya mita 121.5 kati ya kimara na kiluvya ziemshabomolewa.

November 20, Tanroads ilitoa notisi ya simu 30 kuwa wananchi wanaomiliki nyumba hizo kuzibomoa au kuondoka kabla haijaanza kuzibomoa.

Meneja wa Tanroads wa mkoa Julius Ndyamkama alisema hawataki kuwaumiza wananchi wao wakati wa sikukuu kwa kuwa ni kipindi cha kupunguza dhambi kwa mwenyezi mungu.

“ hatuna mpango wa kuwafanya wananchi wasifurahie sikukuu yao. Hiki kipindi cha majaajilio bwana. Tunataka tupunguze dhambi kwa mwenyezi mungu alisema.

Meneja huyo alisema licha ya kuwa wametoa notisi kwa wananchi mpaka desemba 20 haimaanishi watawavunjia nyumba zao kwa kuwa hata wao wana huruma.

Comments


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page