UJENZI WA NJIA SITA BARABARA DAR WAIVA
- Khalidi
- Dec 7, 2017
- 2 min read

Ujenzi wa njia sita katika barabara ya Morogoro yenye kilometa 16 kutoka Kimara, Dar es salaam hadi Kibaha mkoani pwani, inatarajiwa kuanza mwisho wa mwenzi huu,
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa barabara (Tanrods), Mhandisi Patrick Mfugale, alisema hayo alipokuwa akizungumza na Waziri wa Ujenzi, Uchukunzi na Mawasiliano, Prof Makame Mbalawa, alipotembelea na kukagua ubomoaji wa majengo ya serikali likiwemo jingo la shirika la Umeme (Tanesco) na nyumba za watu zilizoko eneo la barabara ili kupisha mradi huo.
Mfugale alisema kazi inayofanyika kwa sasa ni ubomoaji wa majengo na nyumba kuanzia Kimara hadi Kiluvya na kwamba ujenzi utaanza mwishoni wa mwenzi huu.
Pia alisema ujenzi huo utafanywa na mkandarasi atakayepatikana na atapewa mapendekezo ya serikali ambavyo inataka ujenzi wa barabara hizo uwe na yeye ataona kama inafaa kwa ajili ya kuhakikisha ujenzi unakuwa wa kisasa.
Sambamba na hilo, alisema ukarabati wa daraja la mbenzi ambalo lilikatika kutokana na mvua kubwa zilizonyesha Novemba, mwaka huu, unaendelea na hadi kukamilika utagharimu sh. Milioni 650.
Alisema mvua hizo pia zilianza kumega barabara hali ambayo ingesababisha usumbufu kwa watumiaji.
Mfugale pia alisema mbali na ujenzi wa njia hizo, mradi huo pia utahusisha ujenzi wa madaraja mengine makubwa nay a kisasa katika maeneo ambako yatahitajika.
Waziri Mmbarawa, mbali na kuipongeza Tanesco kwa kazi nzuri na kubwa inayoendelea ya kubomoa jingo lake, alisema lengo la serikali ni kuhakikisha barabara hizo zinajengwa ili kuwaletea wananchi maendeleo.
Akiwa eneo la Kimara Temboni, aliwaeleza wananchi kuwa mbali na njia hizo sita, pia wamejenga barabara ya mtaani kwa kiwango cha lami itakayotokea katika Kimara mwisho na kuendelea kupunguza msongamano barabara kuu.
“Tutajenga na barabara hii ya mtaani ambayo kwanza itasaidia wananchi wengine wasiingie eneo la barabara na kuanza kujenga lakini pia itawarahisishia shughuri zenu wakazi wa maeneo haya kwa sababu itatokea Kimara mwisho lengo la serikali ni kurahisisha maisha ya wananchi kwa kuondokana na adha kubwa ya usafiri waliyokuwa wakiipata alisema Prof. Mbarawa.
Pia aliahidi kuwa serikali itahakikisha barabara zote nchini zinapitika bila vikwanzo vya aina yoyote.
Naona wananchi waliojitokenza katika ziara hiyo, mbali na kushukuru serikali kuwaletea maendeleo katika maeneo yao, waliomba kupewa maeneo ya kujihifadhi wakati wakitafuta makazi ya kudumu.
Comments