STRAIKA WA TP MAZEMBE ATUA MSIMBAZI
- Khalidi
- Dec 7, 2017
- 1 min read

Kikosi cha Simba kinaendelea na mazoezi yake ya kujiandaa na mechi zake zijazo za ligi kuu bara zilizobakia baada ya ligi hiyo kusimama kwa muda kupisha michuano ya chalenji inayoendelea kutimua vumbi huko nchini Kenya.
Katika mazoezi hayo yanayofanyika kwenye uwanja wa chuo cha polisi kurasini Jijini Dar es salaam kuna mchezaji mpya kutoka nchini Zambia ambaye amekuja kufanya majaribio akitokea timu ya Zesco ya nchini humo.
Mchezaji huyo ambaye anajulikana kwa jina la Jonas Sakuhawa ambaye pia amewahi kuzitumikia timu za TP Mazembe ya DR kongo , FC Lorient na Ufaransa na Ali merrikh ya Sudan, amezua balaa katika mazoezi hayo baada ya uwezo wake kuwa gumzo kwa kila mtu aliyehudhuria mazoezi hayo.
Uwezo wake mkubwa wa kupiga mashuti lakini pia kumiliki mpira uliwavutia baadhi ya viongozi wa simba waliokuwa wakifuatilia mazoezi hayo.
Hata hivyo kocha msaidizi wa Simba Djuma Masoud ambye alipewa jukumu la kumwangalia mchezaji huyo kama anafaa kuitumikia klabu hiyo amesema kuwa kwa muda mchache aliomuona anaonekana ni mchezaji mzuri lakini bado unahitajika muda zaidi wa kuweza kupima vizuri kiwango chake
Comments