top of page

RATIBA KAMILI RAUNDI YA PILI AZAM SPORTS FEDERATION CUP YANGA NA SIMBA WAPATA VIBONDE

  • Rehema
  • Dec 7, 2017
  • 2 min read

Mabingwa watetezi, Simba SC watamenyana na Green Worriers, zote za Dar es Salaam katika mchezo wa Raundi ya Pili ya Kombe la Azam Sports Federation kati ya Desemba 20 na 25 mwaka huu Jijini.

Mahasimu wao, Yanga watamenyana na Reha FC katika hatua hiyo inayoshirikisha jumla ya timu 64, wakati Azam FC watamenyana na Area C ya Dodoma Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Katika droo iliyopangwa leo studio za Azam TV, Tabata mjini Dar es Salaam, ikiongozwa na wachezaji nyota wa zamani nchini, makipa Steven Nemes, Mwameja Mohammed, beki Kenneth Mkapa na mshambuliaji Bitta John, washindi wa pili wa msimu uliopita, Mbao FC watamenyana na Makanayagio FC ya Rukwa.

Ruvu Shooting watakuwa wenyeji wa Madini FC, Abajalo wataikaribisha Tanzania Prisons, Njombe Mji wataikaribisha Mji Mkuu, Boda Boda FC ya Arusha watakuwa wenyeji wa Singida United na Mwadui FC wataikaribisha Pepsi FC.

Gwiji wa soka nchini, Kenneth Pius Mkapa (kushoto) akionyesha karatasi inayomtambulisha mpinzani wa Yanga, Reha FC. Kulia ni gwiji mwingine, Bitta John aliyeichagua Yanga

RATIBA KAMILI RAUNDI YA PILI AZAM SPORTS FEDERATION CUP.

Ruvu Shooting Vs Madini FC

Abajalo Vs Tanzania Prisons

Njombe Mji Vs Mji Mkuu

Singida United Vs BodaBoda

Mwadui FC Vs Pepsi

Maji Maji FC Vs New Generation

Boma FC Vs Ndanda FC

Stand United Vs AFC Arusha

Burkina Faso FC Vs Lipuli FC

Green Worriers Vs Simba SC

Azam FC Vs Area C

Yanga SC Vs Reha FC

Mbeya City Vs Ihefu

Villa Squad Vs Mtibwa Sugar

Kagera Sugar Vs Makambako

Makanayagio Vs Mbao FC

JKT Mlale Vs KMC

Ambassador Vs JKT Oljoro

Mshikamano Vs Polisi Tanzania

Rhino Vs Alliance

Ashanti United Vs Friends Rangers

Toto Africans Vs Eleven Stars

Maji Maji Rangers Vs Mbeya Kwanza

Milambo FC Vs Buseresere FC

African Lyon Vs Kiluvya United

Biashara United Vs Mawenzi Market

Mvuvumwa Vs JKT Ruvu

Coastal Union Vs Dodoma FC

Polisi Dar Vs Mgambo JKT

Kariakoo United Vs Transit Camp

Shupavu Vs Real Moja Moja

Mufindi FC Vs Pamba SC

Comments


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page