top of page

MO AANZA KAZI SIMBA, ASHUSHA BUNDUKI NNE DIRISHA DOGO.

  • Khalidi
  • Dec 7, 2017
  • 1 min read

Bilionea Mohammed Dewji “Mo” jumapili iliyopita alitangazwa kuwa mwekezaji mkuu wa klabu ya simba baada ya kushinda kwa hisa asilimia 50 kwa dau la sh bilioni 20 alizoweka mezani na tayari ameshaaanza kazi ya usajili.

Mara baada ya kutangazwa Mo aliahidi mambo mengi ambayo ataifanyia klabu hiyo ndani ya kipindi kifupi na kirefu hata hivyo kwa kaunza tayari ameutaka uongozi wa timu hiyo kuhakikisha unatafuta wachezaji katika kipindi cha dirisha dogo la usajili .

Habari za kuaminika kutoka ndani ya zimedai kuwa ‘Mo’ amefikia hatua hiyo baada ya kupata taarifa za benchi la ufundi la simba chini ya kocha mkuu Mcameroon, Joseph omog akisaidiana na mrundi, Djuma Masoud liliutaka uongozi wa klabu hiyo kusajili wachezaji wanne ili kukiimarisha kikosi cha timu hiyo kwa ajili ya ligi kuu na michuano ya kimataifa.

“Benchi letu la ufundi lilitutaka tutafute wachezaji wanne ambao ni kipa, beki wa kati, winga pamoja na mshambuliaji kutokana na upungufu waliouona kwenye mechi zetu zilizopita.

“ kwa hiyo hiyo baada ya Mo kutangazwa, ametutaka benchi la ufundi kuhakikisha tunatafuta wchezaji haraka iwezekanavyo wenye uwezo mkumbwa ili kuziba nafasi hizo tulizotakiwa tuzizibe.

“ kwa hiyo hivi sasa tupo katika harakati na tutahakikisha tunaitumia ipasavyo nafasi hiyo kwa ajili ya kupata wchezaji watakaotusaidia kutimiza malengo yetu ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu lakini pia kufanya vizuri katika michano ya kombe la shirikisho Afrika”

Comments


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page