top of page

Kaburi la Ivan Semwanga limekutwa limefukuliwa.

  • Khalidi
  • Dec 7, 2017
  • 1 min read

Ivan Semwanga ambaye sio tu alikuwa mtu maarufu Nchini Uganda lakini pia Nchini Tanzania kwani alishawahi kuwa mume wa Mke wa Diamond Zari. Kifo chake kilishtua watu wengi ndani na nje ya mipaka ya Uganda.

Mazishi ya Ivan yalikuwa ya kifahari na moja kati ya mambo ya kukumbukwa ilikuwa ni marafiki zake ambao walitupia fedha wakati wa mazishi yake. Kaburi hilo limekutwa limefukuliwa kwenye upande mmoja na kuamsha fikra kuwa kuna uwezekano mkubwa kuwa waliofukua walikuwa wamelenga kuiba fedha ambazo rafiki wa Marehemu Ivan walitupa wakati wa mazishi.

Ufukuaji wa makaburi kwa lengo la kuiba Vito au vitu vingine vya thamani si mgeni maeneo mengi duniani ambapo makaburi mengine ya kifahari huwa yawekwa kwenye maeneo yenye ulinzi mkali kuepuka wazi ambao kwao hawana heshima wala haya kuiba kwenye kaburi.

Comments


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page