top of page

WAZIRI WA JK ASHINDWA KUTETEA KITI

  • Khalidi
  • Dec 5, 2017
  • 1 min read

Waziri wa zamani wa mifugo na Uvuvi DK. Titus Kamani (picha kutoka Maktaba)

Waziri wa zamani wa mifugo na Uvuvi katka serikali ya awamu ya nne na Mbunge wa Busega mkoani Simiyu, DK. Titus Kamani, ameshindwa katika uchaguzi wa Mwenyekiti (CCM) wa mkoa huo.

Katika uchaguzi huo uliosimamiwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Jery Silaa, DK. Kamani alikuwa akiwania nafasi hiyo na wanachama wengine wawili Jonathan Mnyela na Enock Yakobo.

Akitangaza matokeo Silaa alitangaza Yakobo kushinda nafasi hiyo kwa kupata kura 338 na Mnyela kura 15 kati ya kura zote zilizopigwa 749 huku mbili zikiharibika.

Kamani ameshindwa kutetea nafasi hiyo ambayo alikuwa ameishikilia kwa miaka mitano, ambapo baada ya kutangazwa matokeo alikubali kushindwa na kumpongeza Yakobo.

“Nawashukuru wote ambao mmenipatia kura, ingawa hazikutosha, nitabaki kuwa mwana CCM muda wote na kukitumikia Chama change kila wakati,” alisema DK. Kamani.

Nafasi ya mjumbe wa NEC taifa alishinda Emmanuel Gungu aliyepata kura 570 dhidi ya Bulengela kura93 na Emmanuel Mbiti kura51.

Kabla ya kuanza upigaji kura, Silaa alisema wagombea watakao shinda katika uchaguzi huo na kubainiwa kuwa waliendesha kampeni zao kwa kutoa rushwa watachukuliwa hatua kali za kinidhamu.

Aidha, alisema wagombea wote ambao wana malalamiko juu ya uendeshwaji wa uchaguzi huo wawasilishe malalamiko baada ya kumalizika kwa uchaguzi ili yafanyiwe kazi mara moja.

Silaa alisema amepokea taarifa kutoka kwa viongozi wa chama kuwa baadhi ya wagombea wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya rushwa, hivyo atakayebainika atachukuliwa hatua za kinidhamu na kisheria.

Aliongea kuwa kunabaadhi ya watu wametumiwa rushwa kupitia miamala ya simu ili wawachague wagombea na kwamba kisheria wanakiuka taratibu na kanunu za sheria za CCM.

Comments


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page