top of page

Polisi Rwanda Kuwapiga Msasa Watanzania

  • Khalidi
  • Dec 5, 2017
  • 1 min read

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Rwanda Emmanuel Gasana akiongea Jambo na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro

Wataalamu wa Jeshi la polisi Rwanda, wanatarajia kuwasili nchini kutoa mafunzo kuhusu namna ya kukabiriana na uhalifu wa mtandao.

Hayo yalielezwa wakati wa mkutano wa pamoja baina ya Mkuu wa Jeshi la polisi (IGP), Simon Sirro na Mkuu wa Jeshi la polisi Rwanda, Emmanuel Gassana.

IGP Gassana na ujumbe wake, waliwasili nchini kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kubadilishana uzoefu na kujadiliana juu ya makubaliano yaliyofikiwa baina ya majeshi hayo mwaka 2012.

Katika maelezo yake, IGP Sirro alisema mkakati wa mafunzo, unalenga kuhakikisha nchi zote mbili zinakuwa salama dhidi ya uhalifu wa mtandao.

“Tunachangamoto ya makosa ya uhalifu wa mtandao na wenzetu ni wanzuri katika eneo hili, hivyo tumekubaliana tupate wataalamu kutoka kwao wafundishe watu wetu ili kuhakikisha wananchi wote katika shirikisho la Afrika Mashariki wanaishi kwa amani na utulivu” alisema IGP Sirro

Kuhusu makubaliano ya mwaka 2012, alisema kwa kiasi kikubwa yanamafanikio kwani wameweza kuthibiti uhalifu hasa katika maeneo ya mipakani. Alisema wakuu wa polisi katika maeneo ya hayo, wamekuwa wakishirikiana katika kufanya operesheni za pamoja na wanaojihusisha na biashara za dawa za kulevya.

Naye mkuu wa jeshi la polisi Rwanda, Gassana, alisema ziara yake imerenga kuimarisha uhusiano na ushirikiano katika kithibiti uhalifu na wahalifu, hususani maeneo ya mipakani.

Comments


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page