Makachero Polisi Uso Kwa Uso Na Lissu Nairobi
- Khalidi
- Dec 5, 2017
- 1 min read

Mkuu wa Jeshi la polisi nchini, IGP Simon Sirro amesema timu ya wapelelezi imetumwa kwenda Nairobi, Kenya kumuhoji dereva wa Tundu Lissu.
Mbali na dereva, timu hiyo pia inafanya mahojiano na Mbunge huyo wa Singida Mashariki (chadema) na mlinzi wake,

Tangu Lissu ashambuliwe kwa risasi 32 na watu wasiojulikana mchana wa Septemba 7, mwaka huu nje ya nyumba yake, Area D mjini Dodoma wakati akitoka bungeni, dereva wake, Simon Bakari amekuwa akitajwa na polisi kama mtu muhimu anayeweza kusaidia upelelezi.
Hata hivyo Bakari amekuwa Kenya tangu siku hiyo pamoja na Lissu ambaye amelazwa kwenye hospitali ya Nairobi baada ya risasi tano kumpata maeneo mbali mbali ya mwili wake.
IGP Sirro alisema ametuma wapelelezi Nairobi baada ya kusikia Lissu amekubali kuhojiwa juu ya tukio hilo na matarajio yao pia ni kuwapata dereva na mlinzi wake.
“Tumetuma watu wetu kwenda kuchukua maelezo yake (Lissu),” alisema IGP Sirro. “Mwanzo tuliomba kwenda lakini chama (Chadema) walikataa. Juzi tumesikia wamesema wapo teyari.”
“Tumetuma vijana wetu wawili kwenda Nairobi kuchukua maelezo yake.”
Alisema lengo kubwa ni kujua mazingira ya shambulio yalikuwaje na kwamba ikiwezekana wampate dereva na msaidizi huyo wa Lissu ili kurahisisha upelelzi wa tukio lenyewe.
“Upelelezi unaingia vitu vingi sana kutompata dereva na mlinzi wake Lissu inashindwa kutupa picha kamili ya tukio,” alibainisha.
“Niwaambie watanzania watuamini, hatupo kwaaajili ya kuona hatumtendei mtu haki, tupo kwaajili ya kutenda haki.
Mara baada ya Lissu kupigwa risasi, Bakari alikuwa mmoja wa watu waliompeleka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dododma na kasha kupanda naye ndege iliyompeleka Nairobi usiku huo kwa matibabu zaidi
Comments