KISHIMBA: BUNGENI HAKUNA FEDHA ZAIDI YA KUNYWA ‘JUICE’ TU
- Rehema
- Dec 5, 2017
- 2 min read

Mbunge wa Kahama mjini, Jumanne Kishimba (CCM),picha na Maktaba
Mbunge wa Kahama mjini, Jumanne Kishimba (CCM), amesema hakuna fedha wala faida yeyote anayoipata wakati akiwa mbungeni kuwawakilisha wananchi zaidi ya kupigiwa saluti, kupeperusha bendela pamoja na kunywa juisi.
Kishimba aliweka wazi kaneno hayo wakati akizungumza na wakazi wa kitongoji cha Namanga ikiwa ni mwendelezo wa mikutano yake ya kuongea na wananchi wa jimbo lake.
Alisema hadi sasa ameshatumia kiasi cha sh. Milioni 59 kutoka katika mfuko wa jimbo kutekeleza miladi mbalimbali ya maendeleo huku kiasi cha zaidi ya Tsh Milioni 150 akitoa katika mshahara wake kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
“Jamani wananchi wa jimbo langu, hakuna kitu chochote ninachokipata bungeni zaidi ya kunywa juisi, kupeperusha bendela kwenye gari na kupigiwa saluti hata nikinyang’anywa kati ya kimojawapo sijui nitabaki na kitu gani,” alisema kishimba ambaye ni mfanyabiasharamaarufu nchini.
Alisema kunamiradi mbalimbali ya maendeleo ambayo imeshatekelezwa kwa kutumia fedha hizo katika kata mbalimbali ikiwemo ya Elimu na Afya hususani katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa kahama pamoja na miradi ya maji katika maeneo mengine ya jimbo lake.
Aidha alisema pesa yote ya mshahara wake pamoja na mfuko wa jimbo lazima wananchi waijue na ni kazi gani ambayo imetekelezeka kwa kutumia fedha hizo, hali ambayo alisema ni tofauti na miaka ya nyuma ambapo viongozi waliopita walikuwa hawaweki hadharani matumizi ya fedha wanazozipata.
Akizungumza kuhusu suala la maji katika jimbo la Kahama Mjini, Kishimba alisema zaidi ya nusu wa wateja wake wa maji wa Kahama wamekatiwa maji na kuongeza kuwa ameshafanya mazungumzo na uongozi wa mamlaka ya maji taka na usafi wa mazingira katika maji wa Kahama (Kuwasa) ili wateja walipe kidogokidogo.
Katika hatua nyingine Kishimba alisema tangu achaguliwe kuwa Mbunge amefanikiwa kuongeza mapato ya ndani ya Halmashauri hiyo kutoka sh. Milioni 200 kwa mwezi hadi sh. Milioni 700.
Alisema jitihada za ukusanyaji wa mapato ya ndani ya halmashauri hiyo hazihitaji kuwabughuzi wananchi, bali ni kuibua vyanzo mbalimbali vya mapato ambavyo vitaisaidia Halmashauri kupeleka huduma za kijamii kwa wananchi.
Kuhusu Afya, Kishimba alisema Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Kahama imeelemewa na wagonjwa kutokana na kuhudumia wagonjwa kutoka katika wilaya nane zilizopo jirani na wilaya ya Kahama.
Alisema ameshatoa zaidi y ash. Milioni 40 kwaajili ya kusaidia mambombalimbali kama vitanda, mitambo ya kuhudumia watoto wanaozaliwa kabla ya muda wao.
Alifafanua kuwa hospitali hiyo inapokea wakimama 40 mpaka 50 wanaokwenda kwaajili ay kujifungua huku vitanda vilivyopo ni saba tu, hali ambayo alisema ni changamoto kubwa katika kitengo cha afya.
Comments