WAZIRI MHAGAMA AWASHA MOTO MBEYA , AWAPA SIKU 30 WAAJIRI WOTE NCHINI KUJISAJILI WCF
- Fahari News
- Sep 1, 2017
- 3 min read

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, ametoa siku 30 kwa waajiri wote nchini ambao hawajasajili, kujisajili katika
Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi (WCF), na kutoa michango kwa wakati, vinginevyo hatua
kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Waziri Mhagama alitoa agizo hilo jijini Mbeya Julai 27, 2017 wakati wa zoezi la ukaguzi wa kushtukiza jijinihumo kuwabaini waajiri ambao bado hawajatekeleza Sheria ya Fidia kwa
Wafanyakazi Sura 263 Marejeo ya Mwaka 2015 kifungu cha 5, ambayo inawataka
waajiri wote kutoka sekta ya Umma na Binafsi, Tanzania Bara kujisajili kwenye
Mfuko huo.
“Mwajiri ambaye hajajisajili kwenye Mfuko,anaweza kufikishwa mahakamani na adhabu ni pamoja na kutozwa faini ya kiasi chafedha kisichozidi shilingi milioni 50 au kifungo kisichozidi miaka 5 jela auvyote kwa pamoja, hivyo nawasihi waajiri kutoka sekta binafsi na umma Tanzania Bara ambao hawajasajili kutekeleza sheria hiyo inayowataka kujisajili WCF katika muda huo nilioutoa.” Alisisitiza Mhe. Waziri Jenista Mhagama.
Katika ziara hiyo ya ukaguzi wa kushtukiza Mhe. Waziri alifuatana na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba naTathmini wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omar, Mkuu
wa Kitengo cha Uhusiano cha Mfuko huo, Bi. Laura Kunenge na Afisa Kazi wa Mkoa
wa Mbeya, Bi. Mary Patrick Mwansisya ambapo taasisi ya kwanza ambayo Mhe. Mhagama
aliikagua ni Hospitali ya K’s iliyoko eneo la Mafyati na St. Aggrey iliyoko Uyole na kubaini kuwa taasisi hizo hazijajisajili katika Mfuko.
Aidha Waziri alitoa siku saba kwa waajiri wote Mkoani Mbeya wapatao 107 ambao bado hawajajisajili ikiwemo Hospitali ya K’s na Shule ya sekondari St. Aggrey kujisajili ndani ya muda huo.
“Mkishindwa kutekeleza agizo hilo maana yake mnatuelekeza kutumia kifungu cha 71(4), cha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi kinachotamka adhabu ya faini ya kiasi cha fedha kisichopungua
shilingi milioni 50, kifungo cha miaka 5 jela au vyote kwa pamoja.” Alisema.
Aidha Waziri Jenista alihimiza kuwa mwajiri anapojisajili na Mfuko pia atimize wajibu wa kisheria wa kuchangia katika Mfuko kwa wakati stahiki. Mhe. Waziri alisema nia ya Serikali ya awamu
ya Tano sio kuwatisha waajiri bali ni kuhakikisha wanafuata sheria ili hatimaye, wafanyakazi wapate haki yao stahiki pindi wanapoumia, kuugua ama kufariki wakati wakiwa wanatekeleza majukumu ya mwajiri wao kwa mujibu wa mkataba wa ajira.
Akifafanua zaidi Waziri alisema, takwimu zilizopo katika Mfuko za kipindi cha mwaka 2015/16 na 2016/17zinaonesha kuna jumla ya waajiri 229 jijini Mbeya na kati yao ni waajiri 107 tu ndiyo waliojisajili katika Mfuko.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Afya na Tathmini wa WCF, Dk. Abdulsalaam Omar alisema Mfuko unamshukuru Mhe. Waziri kwa kushiriki katika ukaguzi huu wa kwanza wa aina yake
kufanyika tangu Mfuko huu uanzishwe mnamo mwaka 2015 na kwamba Mfuko utasimamia
na kutekeleza maagizo ya Mhe. Waziri.
"Kwa kipindi chote hicho Mfuko umekuwa ukijikita zaidi katika kutoa elimu kwa wadau mbalimbali wakiwemowaajiri ili waweze kuelewa umuhimu wa kujisajili katika Mfuko na faida ambazo
mwajiri na mfanyakazi atazipata pindi anapoumia, kuugua au kufariki wakati akitekeleza majukumu ya mwajiri,” alisisitiza Dkt Omar.
Akifafanua zaidi, Mkurugenzi huyo alisema katika kazi ya uelimishaji kwa kipindi cha mwaka 2016/2017 Mfuko ulitoa elimukwa waajiri wapatao 4,901 kuhusu haki na wajibu lakini pia kuelewa sheriakuhusu wajibu wa waajiri kujisajili katika Mfuko. Aidha Mfuko umekuwa ukitumia
njia mbalimbali kama vile vyombo vya habari, semina lakini pia kwa kuwaandikia
waajiri kuhusu umuhimu wa wao kutekeleza sheria hiyo kwa kujisajili katika
Mfuko na kutoa Michango kwa wakati kama ambavyo sheria inaelekeza.
Dkt Omar alisema Mfuko ulianza kutekelezamajukumu yake tarehe 1 Julai 2015 kama ilivyoelekezwa katika tangazo la Serikali Na. 169/2015 ambapo majukumu hayo ni pamoja na kusajili waajiri, kukusanya michango na kulipa fidia stahiki.
Tayari Mfuko umeanza kulipa fidia kwawafanyakazi walioumia, kuugua ama kufariki kuanzia tarehe 1 Julai 2016.
Ili mfanyakazi aweze kulipwa fidia, nilazima mwajiri wake awe amechangia katika Mfuko, hivyo waajiri wanao wajibu kisheria chini ya Vifungu vya 71 – 78 vya Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi
kujisajili, kuwasilisha michango, kutoa taarifa ya matukio ya ajali na magonjwa
yatokanayo na kazi pamoja na kuwasilisha mapato ya mwaka." Alifafanua Dkt.
Omar.
Naye Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano cha Mfuko huo, Bi. Laura Kunenge alisema, "Tamko alilotoa Mhe. Waziri wetu litakuwa chachu kwa waajiri wengine nchini kujiunga na Mfuko kwa kujisajili na kuwasilisha michango kwa wakati na hivyo kuwezesha kufikia lengo la Mfuko la kulipa Fidia Stahiki kwa wakati",alisema.
Bi. Kunenge pia alisema, Ofisi za WCF ziko wazi na kwamba huduma za Mfuko huo zinapatikana kila mkoa hapa Tanzania Bara ambapo Maafisa Kazi wa Mikoa ndio wanafanya kazi kwa niaba ya Mfuko kwa sasa.
Comments