Yondani kuikosa mechi ya Tz prison
- khalidi
- May 9, 2018
- 1 min read

Beki wa Yanga Kelvin Yondan anatarajiwa kuuukosa mchezo wa Yanga dhidi ya Tanzania prisons kutoka na zuio la bodi ya Ligi kuu la kutoruhusiwa kucheza mchezo wowote wa ligi kuu mpaka swala lake la utovu wa nizamu litakapo jadiliwa na kamati ya Nidhamu
May 3 bodi ya Ligi ilitoa zuio la Yondani kuzuiwa kushiriki katika mchezo wowote mpaka kamati ya nidhamu itakapo keti na kujadili swala lake
Yondani alikutwa na kosa la kumtemea mate Beki wa Simba Sc Asante kwasi kwenye mchezo wao dhidi ya Simba uliopigwa april 29 ambapo Yanga walifungwa goli 1-0
Hii itakuwa ni mara ya pili kwa beki huyo wa kati wa Yanga, Kelvin Yondani kuukosa mchezo wa ligi kuu kwa makosa ya nidhamu uwanjani
Baada ya kuukosa mchezo dhidi ya Ruvu Shooting ya Ligi Kuu Bara uliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kutokana na kutumikia adhabu ya kadi tatu za njano alizozipata kwenye mechi zilizopita za ligi kuu zilizopita
Comments