WAWILI WAFARIKI DUNIA KWA KUANGUKIWA NA UKUTA
- Admin
- Apr 11, 2018
- 1 min read

Watoto wawili wa familia moja, Wilayani nyamagana, mkoani hapa wamefariki dunia baaada ya kuangukiwa na ukuta wa nyumba yao wakati wakiwa wamelala.
Akithibitisha kutokea tukio hilo usiku wa kuamkia jana, Kamanda wa Polisi mkani hapa, Naibu Kamishna Ahmed Msangi, aliwataja waliofariki dunia kuwa ni Mariam Simon (4) na Mussa Baraka(2) na wengine watatu waliojeruhiwa aliwataja kuwa Linda Likuva (68), Ndabaka Samsoni (24) na Samson Simoni (5), wote wakiwa ni ndugu.
Kamanda Msangi alitoa wito kwa wananchi waliojenga nyumba za matofari ya tope kuhakikisha wanaboresha nyumba zao kwa saruji na kuacha kujenga maeneo ya mitaro ya maji ili kuepusha madhara yanayoweza kutokea.
Alisema chanzo kikubwa cha tukio hilo ni mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia juzi ikiwa imeambatana na upepo mkali na kusababisha msingi wa nyumba kutitia na ukuta kuanguka . majeruhi wamelazwa katika hospitali ya wilaya hiyo, Butimba huku miili ya marehamu ikihifadhiwa katika hospitali hiyo.
Suzana Emmanuel ni miongoni mwa mashuhuda na waokoaji wa tukio hilo, alisema walitoa msaada kwa kuwabadilisha nguo majeruhi.
Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo, DK. John Chagula, alithibitisha kupokea miili ya watoto wawili waliofariki katika tukio hilo na majeruhi watatu ambao wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali hiyo na hali zao za afya zinaendelea vizuri.
Comentarios