top of page

KISA CHA SIMU MBILI BUNGENI

  • Writer: Admin
    Admin
  • Apr 11, 2018
  • 1 min read

Bunge limesema kuwa chanzo cha Moshi iliyotokea juzi usiku ndani ya Bunge ni kifaa cha kielektroniki

Cha kuchaji Simu ya mkononi (Power bank) na kwamba ulisababisha harufu kali na kutanda moshi katika ukumbi wa Bunge; hasa upande wa kulia wa kiti cha spika.

“Kwa mujibu wa maelezo ya askari wa Bunge mlipuko ulitokea kwenye power bank ambayo ilikuwa ikichaji simu mbili kwa wakati mmoja kwenye droo ya meza ya mbunge Richard Mbogo,” alisema.

Alibainisha kuwa kifaa hicho kiliteketea kwa moto na kilianguka chini na kuunguza zuria na pembeni mwa kiti cha mbunge huyo.

“Katika tukio hilo hakukuwa na majeruhi isipokuwa baadhi ya wabunge walipata mshtuko na baadhi walikimbia nje ya ukumbi wa Bunge na waliobaki ndani ya ukumbi walipaliwa na moshi na kuanza kukohoa,” alisema.

Naibu Spika, alisema kutokana na hali hiyo ilimlazimu Mwenyekiti wa Bunge Mussa Zungu kuahirisha kikao cha bunge.

Akiomba muongozo kwa Spika, mbunge wa Viti maalum (Chadema), Lucy Mollel alisema haelewi ni kwa nini moshi ulitokea ndani na hakuna kifaa cha kiashiria moshi huo.

“Nilitegemea kungekuwa na alarm (tahadhari) za kutustua sisi huku ndani,” alisema Mollel na kwamba “niliona ni jambo very serious (kubwa sana) lakini sijaona kifaa cha kuashiria.”

“Na tangu tumekuja humu ndani, hatujapewa eneo ambalo tunaweza kukutana kama moto ukitokea na tutatokaje.

Kufuatia muongozo huo, Naibu Spika huyo alisema vifaa hivyo vipo na suala hilo linachukuliwa na linafanyiwa kazi na wataangalia namna ya kupewa maarifa linapotokea jambo la aina hiyo watokaje na kwenda kusimama.


 
 
 

Comments


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page