top of page

RIPOTI VIPIMO VYA NABII TITO RASMI KORTINI

  • Writer: Admin
    Admin
  • Apr 6, 2018
  • 1 min read

Kesi inayomkabili Nabii Tito Machibya maarufu ‘Nabii Tito’, hatima yake kujulikana Aprili 13 mwaka huu, baada ya mahakama ya wilaya ya Dodoma kupokea taarifa za kitabibu jana.

Mahakama ya wilaya ya Dodoma jana asubuhi imepokea taarifa ya vipimo vya kitabibu vya Tito Nabii Tito, ilivyokuwa imeviagiza awali vya kupimwa magonjwa ya akili katika taasisi ya magonjwa ya akili ya isanga mkoani Dodoma.

Jana hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Dodoma, James Karayemaha, alisema atapitia na kutoa maamuzi Aprili 13, mwaka huu.

Hakimu huyo alisema kuwa alipoke taarifa ya kitabibu kuhusu mtuhumiwa huyo leo (jana) asubuhi, hivyo nitaipitia ili Aprili 13, mwaka huu niweze kuitolea maamuzi,” alisema karayemaha.

Nabii Tito jana alihudhuria mahakamani akitokea mahabusu ya gereza la Isanga baada ya kutofikishwa kortini hapo mara mbili mfululizo.

Kutokana na mshtakiwa huyo kutofikishwa mahakamani, Hakimu Karayemaha alimwagiza Mkuu wa gereza la Isanga kuhakikisha Nabii Tito anafikishwa mahakamani jana kusikiliza kesi inayomkabili.

Nabii tito amerudishwa rumande hadi Aprili 13, mwaka huu ripoti ya kitabibu itakapowekwa hadharani.

Nabii Tito anashtakiwa kwa kosa la kutaka kujiua kwa kujikata na wembe na kujijeruhi kwenye maeneo ya tumbo Januari 25, mwaka huu katika mtaa wa ng’ong’ona alipokwenda kukamatwa na polisi.

Baada ya kufikishwa mahakamani, Nabii Tito alidai kuwa ana matatizo ya akili, hivyo mahakama ilimwamuru afanyiwe vipimo vya kitabibu katika Taasisi ya wagonjwa ya akili ya Isanga mkoani hapa.


 
 
 

Comments


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page