top of page

HOFU CHAMA KIMOJA KWA UPINZANI

  • Writer: Admin
    Admin
  • Apr 6, 2018
  • 2 min read

Wabunge waupinzani wameeleza hofu yao juu ya Tanzania kuwa hatarini kurejea katika mfumo wa chama kimoja cha siasa iliuacha mwaka 1992.Wakichangia bungeni mjini hapa jana mchana hoja ya makadirio ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka ujao wa fedha iliyowasilishwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, wabunge watatu wa upinzani walieleza hofu hiyo.Wabunge hao ni Cecilia Pareso (Viti Maalum, Cadema), Peter Lijualikali (Mvomero, Chadema) na Yusuf Salim Hussein (Chambani, Cuf).Katika mchango wake, Pareso alidai tangu kuingia madarakani kwa serikali ya awamu ya tano, kumekuwa kukionekana jitihada za kuua vyama vya upinzani kwa kuvinyima haki zake za msingi.Alisema vyama vya siasa vinatakiwa kufanya siasa ili kuhakikisha vinaendelea kupata wanachama kwa kadri miaka inayoendelea.

Alisema ili vyama viendelee kupata wanachama vianalazimika kunadi na kueleza sera zake na kuwawezesha wananchi kujiunga navyo.Wakati Pareso akiendelea kuchangia, Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga (CCM), alisimama na kumkatisha akiomba kumpa taarifa kuwa kunadi sera mwisho wake ni kipindi cha kampeni tu na kuhoji upinzani iruhusiwe kunadi sera gani wakati sasa CCM ndiyo inayotekeleza sera zake.Hata hivyo, alipopewa nafasi na mwenyekiti wa Bunge, Najma Murtaza Giga kumjibu Mbunge huyo wa CCM, Cecilia alisema hana sababu ya kumjibu na kuendelea kueleza kuwa ni kulidanganya taifa kwa kuwaambia kuwa vyama vya siasa vinaendelea na kufanya kazi huku wamebana mikutano ya hadhara.“Utaendelea kupima kuwa vyama vya siasa vinafanya kazi kama hakuna mikutano ya hadhara? Vyama vya siasa ni kama makanisa, leo mtu anajiunga kesho anatoka,” alisema.Kauli hiyo ya Pareso ilimwinua kitini Mbunge wa Kasulu Vijijini, Vuma Augustino (CCM), ambaye alisema mikutano haijakatazwa kwa kuwa wabunge na madiwani wanatakiwa kufanya katika maeneo yao. “Wataendelea kuvuna wanachama. Ukiangalia wako wanachama wengine wanataka kujiunga na vyama wamevuna mpaka mbunge aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu (CCM),” alisema.


 
 
 

Bình luận


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page