MBOWE KIGUU NA NJIA POLISI
- David
- Mar 5, 2018
- 2 min read

Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo , Freeman Mbowe leo ataongoza viongozi wengine sita wa Chadema kwenda kituo kikuu cha polisi kanda ya Dar es salaam kama walivyoagizwa Jumatatu iliyopita.
Akizungumza na waandishi wa habari kituoni hapo Februari 27, Mbowe alisema aliagizwa kurudi tena leo kwa mahojiano, baada ya kuripoti siku hiyo kuitikia wito wa polisi.
Februari 20, polisi Kanda maalumu ya Dar es salaam aliagiza kukamatwa viongozi saba waandamizi wa Chadema akiwamo Mbowe.
Wito huo ulikuja siku chache baada ya tukio laa kuuawa kwa mwanafunzi wa chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini.
Akwilina aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa ndani ya daladala eneo la Mkwajuni, Kinondoni jijini Dar es salaam wakati polisi wakiwatawanya wafuasi wa chadema waliokuwa wakiandamana kwenda ofisi za mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kudai viapo vya mawakala wao.
Viapo hivyo vilikuwa kwaajili ya uchaguzi mdogo wa ubunge wa Februari 17, katika jimbo hilo.
Viongozi wengine wa chadema waliotakiwa kuripoti na waliofika kituoni hapo siku hiyo na Mbowe ni Naibu Katibu Mkuu wa Zanzibar, Salim Mwalimu na wabunge wanne wa chama hicho Halima Mdee (Kawe), John Heche (Tarime Vijijini), John Mnyika (Kibamba) na Esther Matiko (Tarime Mjini).
Pamoja na viongozi hao sita, polisi pia waliingiza kujisalimisha kwa katibu mkuu wa Chadema, DK Vicent Mashinji ambaye hakuwepo Jumatatu iliyopita kutokana na udhuru wa safari, kwa mujibu wa Mbowe.
Kabla ya kujisalimisha, Mbowe alizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya Chadema na kusema wanaliheshimu jeshi la polisi kwa kuwa wanaheshimu sheria za nchi lakini akadai kuwa wanajua jeshi hilo linapanga nini juu yao.
Katika mkutano huo Mbowe pia alizungumzia matukio mbalimbali ya kisiasa likiwamo la maandamano ya wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la kinondoni, utendaji wa serikali, hukumu ya kifungo cha miezi mitano gerezani dhidi ya Mbunge wa Mbeya ,Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ (Chadema).
Kiongozi huyo wa kambi rasmi ya Upinzani Bungeni pia alizungumzia tukio la kutumika kwa risasi wakati wa maandamano ya Kinondoni, akibainisha kuwa chama chao kimefungua kesi ya kutaka polisi waliotumia risasi hizo wafikishwe mahakamani na kesi hiyo itasikilizwa kesho.
Wakati mbowe akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya nje, John Mrema alitangaza kuwa mmoja wa mawakili wao wamewajulisha kuwa polisi wamepinga kufika kwenye ofisi za makao makuu ya Chadema kwa lengo la kuwakamata.
Tangazo hilo, lilimlazimu Mbowe kukatisha mkutano huo na kutangaza kuanza safari kuelekea kituo cha polisi walikowasili saa 6:50 mchana.
Comments