KAGAME: RWANDA NDOGO LAKINI TUNAPOKEA WAHAMIAJI
- Fahari News
- Jan 23, 2018
- 1 min read

KAGAME: RWANDA NDOGO LAKINI TUNAPOKEA WAHAMIAJI
Rais wa Rwanda, Paul Kagame amesema, hakuna nchi yenye eneo dogo kiasi cha kushindwa kuhifadhi watu, hivyo nchi hiyo itapata sehemu ya kuhifadhi wahamiaji waafrika na itawapa maisha mbadala yenye utu badala ya kuuzwa kwenye soko la watumwa au kuzama baharini.
Kwa mujibu wa Rais Kagame, nchi hiyo itaendelea kuwa teyari kutoa msaada kwa wahamiaji na ikiwa muhimu itawapa makazi kwa watakaokuwa tayari kuishi Rwanda.
“Hakuna nchi ambayo imewahi kuwa ndogo na kutoweza kuhifadhi watu wake na ambao tumekuwa tukujaribu ni kuonesha kwamba, Wanyarwanda wote na waafrika wengine kama wangekuja huku tungetafuta sehemu kwaajili yao,” alisema.
Akaongeza, “ Kwa kweli, sehemu ya kwanza ya mioyoni mwetu, halafu, sehemu ya pili ile inayoonekana inayoweza kusimamiwa kwa namna mbalimbali.”
Aliyasema hayo katiika kituo cha mikutano cha Kigari wakati waa hafla ya chakula cha mchana inayofanyika kila mwaka kwa mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao nchini humo.
Rais Kagame amesema, Rwanda itashirikiana na Umoja wa Afrika (AU), nchi nyingine, na taasisi duniani kushughulikia tatizo la wahamiaji na kuzuia lisiendelee siku zijazo.
Comments