DIAMOND KUJENGA KIWANDA RWANDA
- Fahari News
- Jan 23, 2018
- 2 min read

Msanii nyota wa muziki wa kizazi kipya, Nassib Abdul ‘Diamond Platinumz’ wa Tanzania, anakusudia kuwekeza nchini Rwanda kwa kujenga kiwanda cha karanga nchini humo. Kijana huyo pia anatafuta nyumba ya kuishi jijini Kigali kwa kuwa jiji hilo ni salama, safi na anamkubali sana Rais Paul Kagame.
Kwa mujibu wa msanii huyo, atakapofungua kiwanda kitatoa fursa za ajira na kwamba lengo la biashara yake ni zaidi ya soko.
“….nitafurahi zaidi kama watu watafurahia bidhaa zangu, lakini zaidi wakipata ajira na kubadili hali ya maisha yao,” alisema wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Kigali. Msanii huyo alikwenda Kigali Ijumaa asubuhi kwa safari ya kibiashara na kijamii. Alisema, wasanii wanapaswa kufanya muziki sit u kuburudisha, lakini pia uwe chanzo cha biashara inayoweza kuwanufaisha watu wengi.
“Kunauwezekano kwa vijana wengi kunufaishwa na biashara zetu (wanamuziki), iwe kwenye kazi na mauzo yetu au hata kutengeneza ajira kwa ajili yao mara kiwanda kikianza kazi,” alisema Diamond. Alisema alikwenda jijini humo kusalimia mashabiki wake mtaani na kuwaonesha kuwa sasa amekua. “Nipo nilivyo ni kwasababu muziki wangu. Nimefanikiwa sana, naushukuru muziki. Kwasasa nina Diamond Karanga, manukato ya Chibu na Wasafi Records. Nataka pia kufungua Wasafi FM na Wasafi TV nchini Tanzania,” alisema Diamond.
Alisema wamepata mafanikio kwasababu ya kufanya kazi kwa bidii, watu anaoshirikiana nao, ubunifu na heshima.
Kupitia vyote hivi nipo tayari pia kusaidia vijana kukuza vipaji vyao view vya kiwango cha juu kuendeleza mziki wa Afrika,’ alisema.
Jumamosi Diamond alikwenda kwenye maeneo mbalimbali ya katikati ya jiji la Kigali kutafuta nyumba ya kununua. Alikwenda kuona nyumba kwenye maeneo ya Nyarugrnge na Kimihurura. “Mashabiki wangu Kigali kila mara wanaiona jukwaani, mimevaa miwani lakini sasa nataka nitembee kwenye mitaa ya Kigali, niwasalimie kuwaonesha kwamba kwa kweli nimekua,” alisema wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Nyota huyo wa muziki aliwasili Kigali asubuhi kwa mwaliko wa taasisi ya Jordan, inayojitolea kusaidia watoto wenye matatizo ya kuona kwenye eneo la Gatsata wilayani Gasabo. Taasisi hiyo ilianzishwa na Vanessa Bahati kusaidia wenye matatizo ya kuona.
Comments