RWANDA KUVUNA DOLA MIL 40 ZA MIKUTANO
- Fahari News
- Jan 9, 2018
- 1 min read

Rwanda mwaka huu inatarajia kupokea wageni 22,300 watakaohudhuria mikutano 25 ya kimataifa inayotarajiwa kuingizia nchi hiyo Dola za Marekani milioni 40.
Taasisi ya Mikutano Rwanda (RCB) imethibitisha kuwepo kwa mikutano hiyo, na pia bodi ya maende Rwanda (RDB) imetoa makisio hayo ya fedha.
Kwa wastani, kila mwenzi kutakuwa na mikutano miwili ya kimataifa nchini humo itakayohudhuriwa na wageni 2000.
Mikutano hiyo itahusu masuala ya miundombinu, afya,uwekaji akiba, uchumi, teknolojia ya habari na mawasilioano (ICT), elimu na ubunifu. katika baadhi ya miezi ukiwemo Mei na Novemba, Rwanda itapokea karibu wageni 4000.
Mkutano wa kuibadilisha Afrika unaoandaliwa na Wizara ya ICT na taasisi ya Smart Afrika, na ule kuhusu uongozi wenye malengo kwa Waafrika wote unaandaliwa na taasisi ya Peace Plan Rwanda inatarajiwa kuwa mikubwa zaidi kwa kuwa inahudhuriwa na wageni 2500 kila mmoja.
Mkutano wa kuibadilisha Afrika unaofanyika Mei, na ule wa uongozi Afrika utafanyiaka Oktoba. Mkutano wa tatu kwa ukubwa mwaka huu utahudhuriwa na wageni 2000. Mkutano huo ni wa tano wa kimataifa kuhusu uzazi wa mpango utafanyika Novemba
Comments