top of page

Tuenzi historia !. Huwezi kwenda mbele na kufanikiwa bila kujua historia.

  • Writer: Admin
    Admin
  • Dec 26, 2017
  • 1 min read

Moja ya mafanikio makubwa kufikiwa na Tanzania kwenye nyanja ya mpira wa miguu ni kucheza fainali za Africa mwaka 1980.

Kati ya wachezaji nguli wa wakati huo alikuwa Athumani Juma Chama, yeye alicheza kwenye timu ya Yanga, pia walikuwepo wakina Peter Tino, Jela Mtagwa, Omar Mahadhi, Zamoyoni Mogella na wengine wengi. Wengi wanaamini kile ndio kilikuwa kizazi cha dhahabu kwa mpira wa Tanzania.

Katika siku za karibuni afya ya beki ya kati bora ambaye mechi ya Yanga na Simba ilikuwa inatoa burudani tosha kati yake na Zamoyoni Mogella, yaani Athumani Chama imekuwa dhohofu na kulazwa hospitali.

Kwa wapenda michezo tumuweke kwenye dua na maombi nguli huyu. Pichani Katibu Mkuu wa Yanga Boniface Mkwassa akimjulia hali.


 
 
 

Comments


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page