Aliyekuwa Waziri SMZ akiri kushiriki Mkutano wa CUF.
- Admin
- Dec 23, 2017
- 1 min read

Aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria wa Zanzibar Abubakar Hamis Bakari alisema kuwa alishiriki katika kuchagua bodi ya udhamini ya chama hicho, alisema hayo wakati akitoa ushahidi kwenye mahakama kuu kanda ya Dar es salaam.
Katika kesi hiyo mbunge wa Malindi Ally Saleh, anahoji uhalali wa wajumbe walioteuliwa na Mwenyekiti wa Chama cha CUF Ibrahim Lipumba na kuidhinishwa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA).
Bakari anadai kuwa bodi iliyochaguliwa 2013 ilipaswa kumaliza mida wake May 2018 na hivi karibuni katibu wa bodi hiyo aliwasilisha maombi ya kuongeza wajumbe kutokana na waliokuwepo kutokuwa na sifa.
Comments