top of page

MAGUFULI ASHUKURU MADHEHEBU YA DINI

  • Khalidi
  • Dec 18, 2017
  • 1 min read

Rais John Magufuli jana aliwashukuru viongozi wote wa dini na waumini wa madhehebu mbalimbali ya dini kwa kuendelea kuliombea taifa ili lidumishe amani na upendo, taarifa ya Ikulu ilisema.

Rais Magufuli alitoa shukrani hizo jana mjini Dodoma ambako yeye na mkewe, Janeth waliungana na waumini wa kanisa kuu la Mtakatifu Paulo wa Msalaba, Jimbo Kuu Katoriki la Dodoma kusali ibada ya jumapili. Akizungumza baada ya ibada hiyo, taarifa ya Ikulu kwa vyombo vya habari ilisema, Rais Magufuli alisema serikali anayoiongoza inatambua juhuddi zinazofanywa na viongozi wa dini katika kudumisha amani na upendo. Aidha, Rais Magufuli aliahidi kuwa serikali yake itaendelea kushirikiana nao katika kujenga Tanzania bora. “Nawaomba viongozi wa madhehebu yote ya dini tuendelee kuliombea taifa letu liwe na amani na upendo na serikali itashirikiana nanyi muda wote,” taarifa iliyotolewa na Gerson Msigwa, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu alimkariri Magufuli akisema.

Taarifa hiyo pia ilisema Padre wa kanisa hilo Fr. Sergio Madinda alimshukuru Rais Magufuli kwa ushirikiano wake na kanisa na pia alimshukuru kwa uamuzi wake wa kuhamishia serikali Dodoma. Katika ibada hiyo, taarifa ya Msigwa ilisema, Rais Magufuli alitoa sh. Milioni tatu kwaajili ya kuchangia ujenzi wa kigango cha Michese na kwaya ya kanisa kuu Mtakatifu Paul wa Msalaba.

Rais Magufuli yupo Dodoma kwa wiki moja iliyopita ambapo akiwa huko amefungua mikutano ya uchaguzi ya Jumuiya za Chama cha Mapinduzi za UVCCM, UWT NA Wazazi kabla ya jana kuongoza kamati Kuu na Halmashauri Kuu za CCM.

Pia alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mkutano Mkuu wa Chama cha Walimu (CWT) ambapo aliahidi kumaliza tatizo la madai ya wanataaluma hao ndani ya muda mfupi, yakihakikiwa kwa umakini

Comentarios


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page