top of page

Nani kumrithi Rais Zuma?

  • Writer: Admin
    Admin
  • Dec 16, 2017
  • 1 min read

Mkutano Mkuu wa 54 wa African National Congress unafanyika wiki hii huju agenda kubwa ikiwa ni nani atarithi uongozi wa chama cha ANC kutoka kwa Rais Jacob Zuma.

Rais Zuma ambaye aliingia madarakani kumrithi Rais Mbeki, amekuwa akiandamwa mno na skendo za ufisadi kwa muda mwingi wa uongozi wake. Kumekuwa na jitihada nyingi za kumvua madaraka na kumburuza mahakamani ambazo zimekuwa zikigonga mwamba.

Kinyanganyiro hiki cha uongozi kinakutanisha watu sita ingawa ni wawili wenye kupewa nafasi kubwa.

Wa kwanza ni mke wa zamani wa Rais Zuma, Nkosazana Dlamini-Zuma ambaye pia amewahi kuwa kiongozi wa AU. Wa pili ni Makamu wa rais Cyril Ramaphosa ambaye ni mmoja wa matajiri wakubwa Nchini Africa ya kusini.

Pamoja na kukwamua kutoka kwenye ubaguzi, wengi wa wananchi wa Afrika ya kusini bado wanaishi kwenye maisha duni huku Nchi hiyo ikiwa ni moja ya Nchi zenye utajiri mkubwa wa mali asili na uchumi mkubwa barani Afrika.

 
 
 

Comments


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page