Kutana na Mkazi wa Njombe aliyetengeneza kaburi lake na wake zake 3
- Admin
- Dec 13, 2017
- 1 min read

Kifo ndio safari ya mwisho hapa duniani na hakuna ambaye ataepuka umauti. Kutokana na ukweli kwamba hakuna anayejua akifa inakuaje anaenda wapi na je atakumbukwaje na waliobaki duniani.
Akiwa amejiwekea lengo la kubaki kwenye kumbukumbu hata akiwa amekufa, mkazi wa Njombe Dr.Mwandolane ameamua kuandaa maisha yake na kumbukumbu yake baada ya kufa. Mkazi huyu amejenga kaburi kubwa ambalo lina ghorofa na unashuka Chini kwenda kwenye eneo maalum alilotengeneza kwa ajili ya maziko.
Haya yote anafanya ili abaki kwenye kumbukumbu vizazi na vizazi. Na kutokana na kuwapenda wake zake basi nao amewaandalia sehemu ya wao pia kuzikwa kwenye kaburi hilo la aina yake.
Hii si mara ya kwanza barani Africa kuwa na makaburi ya aina hii. Kuangalia kaburi hili ingia kwenye you tube channel ya Fahari News kuona jinsi kaburi hilo lilivyojengwa. Subscribe kwenye channel yetu ili upate habari Kila zinapotufikia ikiwemo habari ya wafungwa wa maisha walioachiwa na Rais Magufuli.
Comments