top of page

ASILIMIA 80 YA WAFANYABIASHARA RWANDA WATUMIA TPA

  • Khalidi
  • Dec 13, 2017
  • 1 min read

Zaidi ya asilimia 80 ya wafanyabiashara kutoka nchini Rwanda, wanatumia Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kusafirisha mizigo kupitia bandari ya Dar es salaam.

Mwenyekiti wa Chama cha Forodha nchini Rwanda, Seka Fred, alisema huo ni mwanzo wa ushirikiano baina ya Rwanda na Tanzania katika matumizi ya bandari hiyo.

“Kama wafanyabiashara, kwa pamoja tumedhamiria kutumia bandari hiyo hadi kufikia asilimia 100 kutokana na mwingiliano wa biashara na ushirikiano mzuri baina ya nchi hizo,” alisema Fred.

Alisema pamoja na kwamba kuna changamoto ya uhaba wa makontena, lakini wanafurahia huduma zinazotolewa na bandari hiyo.

Makamu wa Rais wa chama cha Mawakala wa Forodha Tanzania (TAFA), Edward Urio, alisema jumuiya ya wafanyabiashara inatarajia kufungua zaidi milango ya kibiashara baina ya nchi za jirani ili kuboresha mwingiliano wa biashara ndani na nje ya nchi.

Alisema bandari ya Dar es salaam imeimarisha ulinzi na usalama, ili kulinda na kusaidia ufanyaji wa biashara kukua zaidi.

“Nimefurahi muungano wa jumuiya ya wafanyabiashara kutoka Rwanda kutokana na maboresho na makubaliano ya kibiashara, inatarajiwa kuwa huko tuendako Bandari ya Dar es salaam itakuwa ni bandari kuu katika nchi zote ndogo ndogo Afrika Mashariki na kuvuka boda zaidi ya hapo,” alisema Urio.

 
 
 

Comments


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page