top of page

AACHIWA KIFUNGO CHA MAISHA AKIWA KWENYE MISA!

  • David
  • Dec 10, 2017
  • 1 min read

Mwandishi wa Fahari News Jackline Charles akifanya mahojiano na aliyekuwa Mfungwa Mr Benson Nyangonda

Msamaha wa Rais Magufuli wa wafungwa hasa wa maisha utaacha simulizi ambazo hazitasahaulika!. Rais Magufuli Jana ameingia kwenye historia baada ya kuachia wafungwa wengi kuliko Rais yeyote aliyetangulia!.

Lakini simulizi za mfungwa aliyehukumiwa kunyongwa zaidi ya miaka 34 iliyopita Mkoani Kagera na kutoka nje akiwa gereza la Ruanda jijini Mbeya ni ya kusisimua!.

Akiwa amehukumiwa kunyongwa akiwa kijana wa miaka 30, Jana ametoka nje akiwa huru akiwa Mzee wa miaka 64!.

Mwandishi wa Fahari news Jaqueline Charles na David Nyembe walipata fursa ya kufanya nae mahojiano ambayo utayaona kwa urefu kwenye you tube channel ya Fahari News.

Kati ya mambo ambayo baada ya kutoka amebaki midomo wazi ni smart phones, bei ya sukari ambayo aliingia gerezani ikiwa senti sasa ni zaidi ya shilingi 2,000, magholofa mengi na mambo mengine mengi. Ingia kwenye you tube channel kuangalia mahojiano ya Baba huyu wa watoto 4!. Msamaha wake aliupata akiwa kwenye misa hapo gerezani na hakuamini alichokuwa anaambiwa na wenzake hadi kiongozi wa gereza alipomfuata na kumwambia!.


 
 
 

Comments


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page