top of page

CCM inayobadilika yamvuta Anna Mghwira

  • Robert Lazaro
  • Dec 8, 2017
  • 1 min read

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh. Anna Mghwira leo amekihama rasmi Chama cha ACT Wazalendo na kuhamia katika Chama cha Mapinduzi (CCM)

Mh. Anna Mghwira amehamia CCM katika Mkutano mkuu wa Jumuiya ya wanawake CCM (UWT), mkutano huo ambao umefunguliwa rasmi na Rais John Pombe Magufuli.

Anna Mghwira katika mkutano unaoendelea hivi sasa amethibitisha kukihama chama hicho cha ACT Wazalendo huku akisema ‘Nimeiona CCM inayobadilika, nimeona juhudi za kila mtu, ninaiona CCM inayoanza kukataa rushwa, nimeiona CCM inayoanza kulipeleka Taifa mbele’

Kabla ya kuchaguliwa na Rais Magufuli kutumikia wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro kama mkuu wa mkoa wa mkoa huo, Mh. Anna Mghwira aligombea nafasi ya uraisi kupitia tiketi ya chama cha ACT Wazalendo katika uchaguzi mkuu uliopita mwaka 2015.


 
 
 

Comments


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page